Kwanini
Mtanzania ufuge samaki
Kuna upungufu mkubwa sana wa protini duniani
na hasa katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania inayotokana kwa asilimia
kubwa na vyakula vya aina ya nyama. Upungufu huu wa protini ambayo ni muhimu kwa
maendeleo ya afya ya binadamu hasa watoto wadogo na vijana wa umri chini ya
miaka 25 husababisha ugonjwa wa kwashakoo kwa watoto.
Pia
matumizi ya samaki na hasa mafuta ya samaki ambayo ndo yanatumika sana
kuwanywesha watoto wadogo yamethibitika kisayansi kuwa yanasaidia sana ukuaji
wa ubongo wa mwanadamu. Lakini pia uwepo wa kiwango kidogo sana cha kolestero
ambayo imeripotiwa kusababisha ugonjwa wa moyo kimepelekea ongezeko kubwa la watu kula samaki.
KWANINI TUNAHAMASISHA WATU WAFUGE SAMAKI:-
-Ongezeko kubwa la uhitaji wa samaki ndani na
nje ya nchi yetu kunako fanya samaki wliopo kutotosheleza mahitaji.
-Kupungua kwa samaki wa asili kwenye mito,
maziwa na bahari kunakotokana na uvuvi wa kupindukia na haramu.
-Urahisi wa kufuga samaki kwa vile hawahitaji
eneo kubwa na chakula kisichokuwa na gharama kubwa.
-Wanauwezo wa kutoa mazao mengi ,faida kubwa,
katika eneo dogo tena ndani ya muda mfupi, uvunaji wa kwanza huanza baada ya miezi 4 hadi 6 hivi na uvunaji wa mwisho kati ya miezi 12.
-Ufugaji wa samaki utaisaidia familia kupata
kitoweo pasipo gharama za ziada na tena itapata protini ya uhakika.
-Upatikanaji wa maji maeneo mengi ya nchi yetu
hasa angalau kwa muda wa miezi michache kwa mwaka hii inatoa fursa ya
kuzalisha samaki katika kipindi ambacho maji yanakuwepo. Lakini pia maeneo
yenye maji ya bomba yanaweza kuzalisha samaki muda wote .
-Samaki wanavumilia sana magonjwa, hata
mazingira duni wanauwezo wa kuishi hasa samaki aina ya perege na kambale.
0 comments:
Post a Comment