UFUGAJI
BORA WA MBUZI WA ASILI
Mbuzi wanaweza kufugwa
kwa gharama nafuu na kuishi katika mazingira magumu kama ya maradhi na ukame
ikilinganishwa na ng’ombe. Kutokana na umbile lao dogo wanaweza kufugwa katika
eneo dogo na pia wanaweza kuhudumiwa na familia yenye nguvukazi na kipato
kidogo. Uzao wa muda mfupi unamwezesha mfugaji kupata mbuzi wengi kwa kipindi
kifupi. Wanyama hao hufugwa kwa ajili ya nyama, maziwa, ngozi na mazao mengine
kwa matumizi ya familia na kuongeza kipato.
Ufugaji bora wa mbuzi
uzingatie kanuni zifuatazo:-
i)
Wafugwe kwenye banda au zizi bora,
ii)
Wachaguliwe kutokana na sifa za koo/aina na
lengo la uzalishaji (nyama au
maziwa)
iii)
Wapatiwe lishe sahihi kulingana na umri na
mahitaji ya mwili,
iv)
Kuzingatia mbinu za kudhibiti magonjwa
kama inavyoshauriwa na mtaalam wa mifugo,
v)
Kuweka na kutunza kumbukumbu sahihi za
uzalishaji; na
vi)
Kuzalisha
nyama au maziwa yenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko
0 comments:
Post a Comment